Pongezi kwa mke wangu Salome

Written on 25/06/2026
Joel Lutomia

Leo ninamshukuru Mungu kwa zawadi ya mke wangu mpendwa.

Nakumbuka siku nilipoamua kwamba nataka kuoa ili nami niwe mwanaume kamili. Haikuwa safari rahisi, lakini ilikuwa safari iliyojaa matumaini, furaha na baraka.

Siku moja nilimwona binti mrembo sana. Macho yangu yalivutiwa naye mara moja. Nikamkaribia kwa heshima na kusema, "Habari mrembo?" Akajibu kwa tabasamu, "Nzuri." Nikamuuliza, "Unaitwa nani?" Akasema, "Salome."

Tulizungumza kwa muda mfupi, na mazungumzo yetu yalikuwa ya kuvutia sana. Mwishoni mwa siku hiyo hatukufanya chochote zaidi ya kubadilishana namba za simu.

Kuanzia hapo, urafiki wetu uligeuka kuwa upendo wa kweli. Tulijifunza kuelewana, kuheshimiana na kusimama pamoja katika nyakati zote. Baadaye tukafunga ndoa takatifu mbele za Mungu na watu, tukasherehekea harusi yetu kwa furaha kubwa.

Mungu akaendelea kutubariki kwa watoto watatu wazuri: Josh, Ruth na James. Wao ni ushuhuda wa upendo wetu na baraka za Mungu katika familia yetu.

Leo, ninapomtazama, Salome, moyo wangu bado unampenda kama siku ya kwanza. Mimi, Joel, ninajivunia kuwa mume wake.